Namna ya kuifadhi namba zako kwenye gmail
Kama umewahi poteza simu yako ama sim card yako unajua ilivo vigumu kurudisha namba zako zote za simu. Nakumbuka zamani watu walikuwa wanaandika namba zao za simu kwenye daftari ama karatasi. Lakini katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia vitu ni rahisi sana zifuatazo ni njia za kuifadhi mawasiliano yako kwenye account yako ya gmail na namna ya kuzirudisha unapokuwa na simu mpya.
angalizo: usisahau Gmail account yako au password yake unapotengeneza account yako ya gmail weka vitu unavyovikumbuka kiurahisi
- Yakupasa uwe na account ya gmail unapokuwa na simu ya android Unganisha na account hiyo hamisha namba zote kwenye account hiyo na unaposave namba mpya akikisha unasave kwenye account hiyo.
- Unaponunua simu mpya ya android unganisha na gmail account yako.
- Kwenye simu ya android nenda "Menu> Setting > Account na minya sehemu iliyoandikwa Sync"
- Bonyeza kwenye "Sync Contact" hii itarudisha mawasiliano yako yote kwenye simu hiyo mpya.
- Angalia kama namba zako zote zimerudi.
Ukifuata hatua hizi hutokuja kupoteza namba zako za simu utakuwa nazo popote pale chamsingi ni kukumbuka account ya gmail na password.
Usisahau kucomment na kudownload App yetu ya smartphone
Kwa watumiji wa Android
👍👇 LIKE US FOR UPDATE FROM US 👍
Comments
Post a Comment